Mwanamke mmoja amemshaki spika wa bunge la seneti Ken Lusaka kwa madai ya kutelekeza majukumu yake ya ulezi.

Kupitia kwa wakili wake Dunstan Omari, mwanamke huyo anadai kuwa Lusaka ambaye ni Gavana wa zamani wa Bungoma amekataa kujukumikia mahitaji ya mwana wao ambaye hajazaliwa.

Omari anadai wawili hao wamekuwa kwenye mahusiano tangia mwaka 2018 hadi mwezi Mei mwaka huu wakati Lusaka anadaiwa kuhepa alipogundua kuwa mwanamke huyo alikuwa amepata mimba.

Mwanamke huyo ameiomba mahakama kumlazimisha Lusaka kumlipa Sh200,000 kila mwezi ili kumlea mtoto wao la sivyo amlipe shiligi million 25 mara moja.

Jaji James Makau ameorodhesha kesi hiyo kuwa ya dharura na kuagiza Lusaka kukabidhiwa stakabadhi za kesi.