Aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga ametoa wito kwa wakenya kushirikiana kumaliza visa vya watoto kupotea, kuuwawa, kujeruhiwa au pia dhulma dhidi ya watoto.

Katika taarifa ya kuadhimisha siku ya mtoto wa Kiafrika tarehe 16 Juni mwaka 2021, Odinga ametaja taarifa za dhulma dhidi ya watoto kuwa za kuvunja moyo na kutaka zikomeshwe mara moja.

Odinga anatoa wito kwa mataifa ya Afrika kutoonyesha watoto mgongo licha ya hali ngumu ya maisha, na badala yake kuwa wa msaada kwao.

Kiongozi huyo aliyepia balozi wa miundo msingi katika muungfano wa AU ametoa wito kwa kila mtu kuwa macho, na kuripoti haraka visa wanavyoshuku vya dhulma dhidi ya watoto.

Matamshi ya Odinga yanajiri huku Kenya ikijiunga na mataifa mengine barani kuadhimisha siku ya mtoto wa Kiafrika.