Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutua amewataka wakosoaji wa naibu rais William Ruto kubadili mbinu na waache kumtaja ovyo ovyo..

Dkt. Mutua amesema wanaomtaja Ruto kila mara mara wanamtafutia umaarufu na badala yake amewataka waangazie maendeleo.

Gavana Mutua amesema haya akiwa Embakasi, Nairobi kupigia debe chama chake cha Maendeleo Chap Chap ambapo amewashauri Wakenya kuacha siasa za ukabila.