Serikali imeonya kwamba huenda ikatangaza vikwazo vya usafiri katika baadhi ya maeneo ya Magharibi na kaunti za Nyanza kudhibiti msambao wa virusi vya corona.

Waziri wa Usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i amesema wanafuatilia kwa karibu msambao wa ugonjwa huo katika kaunti hizo kabla ya kutoa mwelekeo baada ya mashauriano.

Hospitali za umma na zile za kibinafsi katika kaunti ya Kisumu zimeripoti idadi kubwa ya wagonjwa wa corona huku kaunti hiyo ikijitahidi kuwapima watu zaidi katika juhudi za kupambana na maambukizi.