Wakenya ambao hawakupata fursa ya kusajiliwa kupata Huduma Namba watapata fursa hiyo hivi karibuni.

Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna amesema awamu ya pili ya usajili huo itaanza hivi karibuni baada ya kukamilisha mipango yote.

Serikali vile vile imewataka Wakenya ambao tayari wamesajiliwa kuchukua kadi zao pindi wanapopata ujumbe wa kuwajulisha kwamba kadi zao ziko tayari.

Oguna amesema kufikia sasa kadi za Huduma Namba zaidi ya milioni tano ziko tayari ila zilizochukuliwa ni milioni tatu pekee.