Wanasiasa wenye tabia ya kuwachochea Wakenya uchaguzi unapokaribia watapigwa marufuku kusafiri Marekani au mataifa mengine ya bara ulaya.
Haya yamesemwa na mwenyekiti wa tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC Kasisi Samwel Kobia ambaye amesema wanashauriana na mabalozi wa mataifa mbalimbali kuwanyima visa viongozi kama hao.
Hii itakuwa ni kuongezea kwa uchapishaji wazi wa majina ya wanasiasa wazushi wanaokosa adabu kwenye mikutano yao ya kisiasa.
Kwenye orodha hiyo wako wabunge Simba Arati wa Dagoreti Kaskazini na mwenzake wa Mugirango Kusini Silvanus Osoro.