Katibu mkuu wa muungano vya wafanyikazi nchini (COTU) Francis Atwoli kwa mara ya nne mfululizo amechaguliwa kuwa mwanachama wa bodi ya kimataifa ya wafanyikazi (ILO) yenye makao yake mjini Geneva, Switzerland.
Atwoli amechaguliwa kwenye mkutano wa mia moja na tisa unaoendelea kwa njia ya mtandao.
Hii ina maana kwamba Atwoli ataendelea kuliwakilisha bara la Afrika kwenye bodi hiyo kuu ambayo hufanya maamuzi kuhusu maswala yanayohusiana na maslahi ya wafanyikazi.
Itakumbukwa kwamba Atwoli mnamo mwezi Aprili mwaka huu alichaguliwa kuhudumu kwa muhula wa tano kwa muungano wa COTU baada ya kukosa mpinzani.