Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amemtaka aliyekuwa Jaji Mkuu Dkt. Willy Mutunga kufunga mdomo kuhusu mjadala unaozingira uhuru wa idara ya mahakama.

Akizungumza kwenye mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Kibwezi Kalembe Ndile, Odinga amesema Mutunga hafai kuzungumzia zogo linaloendelea kuhusu uapisho wa majaji sita kwa sababu aliwanyima haki kwenye kesi ya kupinga uchaguzi wa urais mwaka 2013.

Waziri huyo mkuu wa zamani vile vile amedai kuwa Wakenya wanafinywa na bajeti ghali kwa sababu maafisa wa ngazi za juu serikalini wanaiba pesa zinazofaa kutumika kwa maendeleo.

Akizungumza kwenye mazishi hayo, gavana wa Kitui Charity Ngilu amewataka Odinga na kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka kuungana tena la sivyo watashindwa na naibu rais William Ruto.