Jaji Mkuu Martha Koome amesisitiza kwamba rais Uhuru Kenyatta ni lazima awateuwe majaji SITA waliosalia baada yake kukataa kufanya hivyo.

Koome akihutubu kwenye hafla ya kuapishwa kwa rais wa mahakama ya Rufaa Daniel Musinga amesema hataki kuingia kwenye mvurugano wowote na afisi ya rais na kumtaka kufanya hivyo haraka upesi.

Akikubali kwamba idara ya mahakama inakabiliwa na wakati mgumu kwa sasa, rais huyo wa mahakama ya upeo vile vile amesema uhuru wa idara hiyo unakabiliwa na tishio la kunaswa na watu fulani ambao hakuwataja na kuwataka majaji na kuulinda.

Itakumbukwa kwamba rais Kenyatta alikataa kuwaapisha majaji hao kwa misingi kwamba maadili yao ni ya kutilia doa hatua ambayo imeibua mjadala mkali nchini rais akijipata akisomewa hata na waliokuwa majaji wakuu Dkt. Willy Mutunga na David Maraga.