Benki ya Dunia imeipatia Kenya mkopo wa Sh80.9b kutumia katika maswala mbalimabli yenye umuhimu.
Katika taarifa World Bank imesema pesa hizo zinatazamiwa kutumika katika kukomboa uchumi uliokwama kutokana na janga la corona sawa na kusaidia kusimamia madeni ambayo taifa hili limekopa.
Kenya inapokea mkopo huo siku moja baada ya waziri wa Fedha Ukur Yatani kuwasilisha makadirio ya bajeti bungeni na kusema kwamba taifa linahitaji mikopo zaidi kufadhili bajeti hiyo inayogharimu Shilingi Trilioni Tatu nukta sita.
Alisema ataliomba bunge ili kuongeza kiwango cha mikopo ya Kenya kupanda na kufikia zaidi ya shilingi trilioni tisa.