Tume ya uchaguzi IEBC siku ya Jumatatu inatazamiwa kuzindua wiki ya kutoa mafunzo kwa umma kuhusu mchakato wa uchaguzi.
Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati anatazamiwa kuongoza zoezi hilo ambalo linalenga kutoa mafunzo kwa mpiga kura kuhusiana na mchakato wa uchaguzi.
Tume hiyo inalenga kutumia mafunzo hayo pia kuelezea umma majukumu yake na mipango yao haswa kuhusu uchaguzi mkuu wa Agosti mwakani.