Kinara wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi anahoji kwamba itakuwa vigumu kutekeleza bajeti inayogharimu Shilingi Trilioni tatu nukta sita kutokana na hali ngumu ya kiuchumi.

Mudavadi ameelezea wasiwasi wake kwamba bajeti hiyo italizamisha taifa kwa madeni zaidi kwa sababu waziri wa fedha Ukur Yatani atahitaji kuomba mikopo ili kuafikia malengo ya bajeti hiyo.

Ameongeza kuwa mwananchi wa kawaida atabeba mzigo zaidi kwa sababu serikali itaongeza ushuru ili kuiwezesha kugharamia bajeti hiyo.

Aidha, waziri huyo wa zamani wa fedha amesema kuwa mapato yatakayokusanywa kupitia ushuru yatapungua kwa kiwango kikubwa kwa sababu Wakenya wengi walipoteza kazi na biashara nyingi kufungwa kwa muda wa mwaka mmoja uliopita kutokana na janga la corona.