Wizara ya afya imezindua mkakati utakaohakikisha kwamba afya ya akili imepewa kipau mbele.

Uzinduzi huo ulioongozwa na katibu msaidizi wa wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi utawezesha usimamizi bora wa afya ya kiakili na kuanzisha mipango itakayohakikisha kwamba hilo limeafikiwa.

Aidha, mkakati huo utahakikisha kwamba Wakenya wamepata matibabu yanahusiana na afya ya kiakili huku serikali za kaunti zikipewa kipau mbele kufuatia kugatuliwa kwa huduma za afya.

Chini ya mpango huo, asasi mbalimbali zitashirikiana huku hatua za kuboresha afya ya akili zikichukuliwa kwa lengo la kuafikia madhumuni haya.