Mahakama ya Leba imefutilia mbali ombi la tume ya huduma za bunge (PSC) lililotaka kesi inayopinga uteuzi wa karani wa Michael Sialai kutupwa nje.

Kesi ya kupinga uteuzi wa Sialai iliwasilishwa mahakamani na mwanaharakati Okiya Omtatah kwa misingi kwamba ilikuwa kinyume cha sheria kumteua tena kuhudumu kwa wadhifa huo kwa kandarasi bila idhini ya bunge ilhali amefikisha umri wa miaka 60.

PSC kwenye kesi yake ilikuwa inahoji kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo jaji Monica Mbaru amefutiia mbali ombi la PSC kwa misingi kwamba mahakama hiyo ina uwezo wa kusikiliza na kuamua kesi hiyo.