Goerge Koimburi na Pavel Oimeke wameapishwa rasmi kama wabunge wa Juja na Bonchari mtawalio.

Wawili hao wameapishwa katika bunge la kitaifa mbele ya spika Justine Muturi.

Koimburi wa chama cha PEP alishinda kiti cha Juja kwenye uchaguzi mdogo baada ya kupata kura 12,159 huku Oimeke wa ODM akishinda uchaguzi wa Bonchari kwa kupata kura 8,049.

Viti vya Juja na Bonchari vilisalia wazi kufuatia vifo vya Francis Waititu na Oroo Oyioka