Watu 148 zaidi wamepatwa na virusi vya corona baada ya kupima sampuli 2,163 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Wizara ya afya inasema hii inafikisha 172,639 idadi ya visa hivyo nchini huku maambukizi yakiwa katika kiwango cha asilimia 6.8%.

Watu wengine 631 wamepona katika muda huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 118,226 huku maafa yakifikia 3,308 baada ya kufariki kwa wagonjwa wengine 21.

Waliopata chanjo ya kwanza kufikia sasa ni 975,835 huku waliopata dozi ya pili wakiwa 13,194.