Polisi wanachunguza mauaji ya mtu mmoja raia wa Uholanzi katika makaazi yake huko Shanzu mjini Mombasa.

Mwili wa Herman Rouwenhorst,55, ulipatwa na Polisi waliojibu simu kutoka kwa mwanamke aliyehitaji msaada.

Polisi kutoka Bamburi walimpata mwanamke mmoja aliyetambulika kama Riziki Cherono akiwa amefungwa.

Ripoti ya Polisi inaonesha kuwa mwili wa marehemu ulikuwa kitandani huku miguu na mikono yake ikiwa imefungwa kwa kutumia kamba na mdomo wake ukiwa pia umezibwa.