Maafa yanayotokana na ugonjwa wa corona yameongezeka na kufikia 3,206 baada ya kufariki kwa wagonjwa 18 zaidi katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amethibitisha maambukizi mapya 142 katika muda huo kati ya sampuli 2,650 zilizopimwa na kufikisha idadi ya visa hivyo nchini kuwa 171,226.

Watu 16 zaidi wamepona na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 117,039 huku kiwango cha maambukizi kikiwa katika asilimia 5.4%.

Wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali kote nchini ni 1,251 huku wanaosghulikiwa numbani wakiwa 4,705.