Mtoto wa siku saba ni miongoni mwa watu 349 waliokutwa na virusi vya corona kati ya sampuli 4,208 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.  

Wizara ya afya inasema hii inafikisha 171,084 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini huku kiwango cha maambukizi kikiwa katika asilimia 8.3%.

Wagonjwa 176 wamepona na kufikisha idadi hiyo kuwa 117,023 huku waliofariki wakifikia 3,188 baada ya kuripotiwa kwa maafa 16 zaidi.

Takriban wagonjwa 1,257 wamelazwa katika hospitali mbalimbali huku wengine 4,704 wakishughulikiwa nyumbani.