Rais Uhuru Kenyatta ametoa hakikisho kwamba serikali itaendelea kutoa mazingira bora kwa biashara kunawiri lengo likiwa ni kubuni nafasi kza azi.
Rais amesema serikali itaendelea kutafuta masoko mapya na kupanua yaliyopo ili kuwawezesha wakulima kuuza mifugo wao kwa bei nzuri.
Kiongozi wa taifa amesema haya alipoongoza ufunguzi wa kichinjio cha Neema kilicho Lucky Summer, Nairobi ambacho ujenzi wake umegharimu Sh300M.
Rais Kenyatta ametaja kuwa ufunguzi upya wa kiwanda cha nyama cha Athi River ni miongoni mwa mikakati ya muda mrefu kuwafaidi wakulima nchini.