Jaji David Musinga amechaguliwa kuwa rais mpya wa mahakama ya Rufaa.

Jaji Musinga anachukuwa nafasi ya Jaji William Ouko aliyeteuliwa kuwa jaji wa mahakama ya upeo.

Uchaguzi huo ulisimamiwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.

Jaji Musinga ambaye aliteuliwa kuwa jaji wa mahakama ya rufaa mwaka 2012 atakuwa mwakilishi wa mahakama hiyo katika tume ya huduma za mahakama JSC.

Katika mahakama ya upeo, Jaji Ouko alijaza nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kustaafu kwa jaji Jacktone Ojwang’.