Wakenya waliopata chanjo ya kwanza ya AstraZeneca wameshauriwa kutokuwa na wasiwasi kuhusu kupata chanjo ya pili.

Hakikisho hili limetolewa na waziri wa afya Mutahi Kagwe ambaye amesema waliopata chanjo ya kwanza lazima wapate ya pili.

Hata hivyo waziri Kagwe amesadiki kwamba Kenya inahitaji chanjo zaidi ili kuwachanja raia wake dhidi ya ugonjwa wa corona.

Ameongeza kuwa upungufu wa chanjo hiyo unaoshuhudiwa kwa sasa katika mengi ya mataifa barani Afrika umesababisha na mapambano dhidi ya janga la corona yanayoendelea nchini India ambaye ni tegemeo kuu.

Kufikia sasa, zaidi ya watu laki tisa wamepata chanjo hiyo huku watu zaidi ya laki mbili wenye umri wa miaka hamsini na nane na zaidi wakipata chanjo hiyo.