Rais Uhuru Kenyatta amemteua rasmi Martha Koome kuwa Jaji Mkuu wa Kenya saa chache baada ya kuidhinishwa na bunge.

Kenyatta amechapisha jina la Koome na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo.

Wabunge kwa kauli moja waliidhinisha ripoti ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu haki na masuala ya sheria (JLAC) iliyoidhinisha uteuzi wake baada ya kumsaili.

Wabunge wameunga mkono ripoti hiyo na kusema jaji Koome anafaa zaidi kumrithi David Maraga kutokana na tajriba na uzoefu wake.

Mwenyekiti wa kamati hiyo aliye pia mbunge wa Kangema Muturi Kigano ameliambia bunge kwamba Jaji Koome alidhihirisha uwezo wa kutekeleza majukumu ya jaji mkuu na haswa kupambana na ufisadi katika idara ya mahakama na pia kutatua mzozo baina ya idara hiyo na afisi ya Rais.

Koome sasa anasubiri uteuzi rasmi kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta kabla ya kula kiapo kuingia afisini.

Koome sasa atakuwa mwanamke wa kwanza jaji mkuu katika taifa la Kenya na kumrithi David Maraga aliyestaafu.