“Hatujafurahia namna maseneta walivyoshughulikia  kutimuliwa kwa Gavana wa Wajir Mohamed Mohamud.”

Ndio kauli ya baraza la magavana ambalo kupitia kwa mwenyekiti wake Martin Wambora limesema kuwa mchakato huo ulikiuka sheria ikiwemo kupuuzwa kwa agizo la mahakama lililozuia kuondolewa kwa gavana huyo.

Baraza hilo limewashtumu maseneta kwa kuwa kigeugeu katika maamuzi yake wakati wa vikao vya kujadili hoja za kuwatimua magavana.

Baraza hilo limesema litaandaa kikao maalum ijumaa hii kujadili maswala hayo na kutoa ripoti

Mohamed Mohamud alitimuliwa kutoka kwa kiti cha gavana baada ya Maseneta 25 kupiga kura ya kuunga mkono kungolewa kwake afisini huku maseneta wawili wakipinga na wengine wanne kutopiga kura.