Afisa mmoja wa Polisi anatazamiwa kushtakiwa leo Jumatatu kwa mauaji ya makanga mmoja huko Ongata Rongai.

Constable Edwin Oscar Okimaru alishikwa Ijumaa na majasusi wa idara ya upelelezi DCI.

Anatuhumiwa kumuumiza Joshua Mungai pamoja na wakaazi wengine wawili alipokuwa anatekeleza masharti ya kafyuu.

Mungai alifariki siku mbili baadaye kutokana na majeraha aliyopata akiwa hospitalini.

Matokeo ya upasuaji yanaonesha kuwa Mungai alifariki kutokana na majeraha ya kifua, kuvunjika kwa mbavu na mifupa kiashirio kwamba aliteswa sana.