Rais Uhuru Kenyatta amemteua rasmi Jaji William Ouko kuwa Jaji wa mahakama ya upeo baada ya kuidhinishwa na tume ya huduma za mahakama JSC.

Ouko anajaza nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kustaafu kwa Jaji Jackton Ojwang’.

Hadi uteuzi, Jaji Ouko amekuwa rais wa mahakama ya Rufaa na alijaribu bahati yake kuwa Jaji Mkuu.