Wakenya wanahimizwa kutoa maoni yao kuhusu makadirio ya bajeti mwaka 2021/2022 yanayotarajiwa kuwasilishwa bugeni mwezi ujao.

Waziri wa Fedha Ukur Yattani ambaye atakuwa anawasilisha bajeti hiyo Juni 10 anawataka Wakenya kutoa maoni yao kabla ya Mei 26.

Bajeti hiyo inatazamiwa kupendekeza mbinu za kuinua tena biashara zilizotatizika na janga la corona na kuinua uchumi ulioathirika na janga hilo.

Balozi Yattani vile vile ameeleza kwamba makadirio hayo ya bajeti yatapendekeza namna ya kupata pesa zitazotumiwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia kwa ushuru.