Wabunge watatu wametakiwa kufika binafsi bungeni Alhamisi hii kwa kudai kwamba wabunge waliopigia kura ya kuunga mkono mswada wa BBI walihongwa.
Spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi amewaagiza watatu hao Moses Kuria (Gatundu Kusini), Ndindi Nyoro (Kiharu) na Mohammed Ali (Nyali) kufika bungeni kutoa mwanga zaidi kufuatia madai hayo.
Mohammed Ali kupitia kwa mtandao wake Twitter alidai kwamba wabunge walihongwa Sh100, 000 ili kupitisha mswada huo.
Kuria, Nyoro na Ali wameagizwa kufika bungeni kujitetea baada ya wenzao kulalamika kuwa wamewachafulia jina kufuatia madai hayo ya kuhongwa ili wapitishe BBI.