Msemaji wa polisi Charles Owino amepewa uhamisho katika mabadiliko yaliyofanywa na inspekta mkuu Hillary Mutyambai.

Owino sasa ni naibu mkurugenzi katika shirika la silaha ndogondogo KNFP huku nafasi yake ikibaki wazi.

Owino amekuwa akitetea maafisa wa polisi kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo mauaji ya kiholela.

Mabadiliko haya yanajiri miezi miwili tu baada ya Owino kusema atajitosa kwenye siasa katika uchaguzi mkuu ujao huku akimezea mate wadhfa wa Gavana wa Siaya.