Idadi ya maambukizi ya corona inazidi kupungua nchini huku visa 356 vikidhibitishwa kati ya sampuli 4,424 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Wizara ya afya inaarifu kuwa hii inafikisha 163,976 idadi ya visa vya ugonjwa huo kufikia sasa.

Idadi ya waliopona imefikia 113,057 kufuatia kupona kwa watu 129 huku maafa yakifikia 2,928 baada ya kufariki kwa wagonjwa 21 zaidi.

Kufikia sasa, watu 921,546 wamepewa chanjo ya corona ikiwemo watu 281,704 walio na umri wa miaka 58 na zaidi; wahudumu wa afya 161,271, walimu 144,434 na maafisa wa usalama 77,772.