Madereva wanaowapata wateja wao kwa njia ya mtandao katika miji ya Nairobi, Mombasa, Kisumu, Nakuru na Naivasha wamesusia kampuni za Uber na Bolt kulalamikia mapato ya chini.

Katibu wa shirika la Digital Taxi Wycliffe Alutalala amekiambia kituo hiki kwamba wamesusia kampuni za Uber na Bolt kutokana na kutoangaziwa kwa matakwa yao licha ya kupanda kwa bei ya mafuta.

Alutatala amesema mgomo huo utaendela kwa muda wa siku 40 ambapo wanatarajia kuwa wateja wao watakuwa wame hamia mitandao tofauti ambayo watakuwa wanatumia.

Madereva hao wanasema wateja wamekuwa wakilipizwa ada za chini na kuwaacha bila hata pesa za kununua mafuta kuendesha biashara hiyo.