Kwa mara nyingine tena jamii ya Wanubi imelalamikia ubaguzi wakati wa kutolewa kwa vitambulisho vya kitaifa uchaguzi mkuu unapokaribia.

Watu kutoka jamii hiyo kupitia kwa shirika la kutetea haki zao la Nubian Rights Forum lililoko Kibra likiongozwa na Shaffie Hussein Ali wanalalama kuwa serikali imewawekea vikwazo wanapopata stakabadhi hiyo muhimu ya kitaifa ikiwemo kuwakagua kabla ya kupewa.

Amesema licha ya kilio chao, serikali imekataa kuwasikiliza na hivyo kufanya vigumu kwa wengi wao kupata kazi kwa kukosa vitambulisho.