Bunge la kitaifa limelitaka lile la Senate kuiga mfano wake na kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI wiki ijayo.

Kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa Amos Kimunya amesema maseneta wanapaswa kupitisha mswada huo ili kutimiza maazimio ya Wakenya kurekebisha katiba.

Naye kiranja wa walio wachache katika bunge hilo Junet Mohammed amewapongaza wabunge kwa kupitisha mswada huo kwa idadi kubwa.

Wabunge wapatao 235 walipiga kura kupitisha mswada huo ikilinganishwa na wabunge 83 waliopiga kura ya LA.