Serikali imetangaza kuwa Ijumaa ya tarehe 14 mwezi huu itakuwa sikukuu.

Katika tangazo kwenye gazeti rasmi la serikali, waziri wa Usalama wa ndani Dr Fred Matiang’i amesema sikukuu hiyo itakuwa ya kutoa fursa kwa waumini wa dini ya Kiislamu kuadhimisha siku ya Id-ul-Fitr.

Siku hii huashiria mwisho wa mfungo wa Ramadan.