Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga wamewaomba wabunge kuweka kando tofauti zao na kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI huku maseneta wakitazamiwa kuupigia kura Alhamisi.

Kwenye taarifa ya pamoja, Uhuru na Odinga wamewataka wabunge kujiunga na Wakenya milioni tatu waliotia saini zao kwenye mswada huo na wanatarajia kushiriki katika kura ya maamuzi kubadilisha katiba hivi karibuni.

Wameongeza kuwa huu sio wakati wa kuendelea kuvutana kuhusu marekebisho kwenye mswada huo kwa sababu hatima ya hayo yote inasalia mikononi mwa raia watakaposhiriki kwenye kura ya maamuzi.

Tayari spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi amezima juhudi za wabunge kuurekebisha mswada huo akisema jukumu hilo sio lao ila ni la wananchi.