Baraza la magavana linalalama kuwa limeshindwa kupambana na janga la corona kwa sababu ya ukosefu wa pesa.

Mwenyekiti wa baraza hilo Martin Wambora amesema bado hawajapokea Sh70.2b ambazo wanadai serikali kuu.

Amesema kukosa pesa hizo kumetatiza pakubwa mikakati ya kupambana na janga hilo la corona.

Wambora anasema kuwa baadhi ya kaunti zimeshindwa kuwalipa wafanyikazi wake mishahara ya hadi miezi mitatu.