Mbunge wa Limuru Peter Mwathi amechaguliwa bila kupingwa kuwa mwenyekiti mpya wa kamati ya bunge la kitaifa kuhusu Usalama.

Mwathi anachukua wadhifa huo uliobaki wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Kiambaa Paul Koinange.

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Wajir Fatuma Gedi alikuwa ameelezea nia yake kujaza nafasi hiyo ila akakosa kutuma maombi yake kabla ya makataa yaliyowekwa.

Kabla ya uteuzi wake, Mwathi alikuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge hilo la kitaifa kuhusu Leba.

Koinange alifariki dunia mwishoni mwezi Machi mwaka huu katika hospitali ya Nairobi alipokuwa amelazwa kutokana na matatizo yanayoambatana na corona.

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imeratibu uchaguzi mdogo wa Kiambaa kuandaliwa Julai 15 mwaka huu.