Mwanamke mmoja nchini Mali amejifungua watoto TISA kwa wakati mmoja.

Madaktari wanasema Halima Cisse, 25, alikuwa ametarajiwa kujifungua watoto SABA na wasemavyo waswahili, mambo ni kangaja na huenda yakaja kwani alizaa watoto TISA wakiwemo wasichana watano na wavulana wanne katika hospitali moja nchini Morocco.

Watalaamu wa afya walishauri mama huyo amepelekwe Morocco mnamo Machi 30 mwaka huu kupata usaidizi maalumu.

Wizara ya afya katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika inaeleza kuwa mama huyo alijifungua watoto hao wote kupitia upasuaji.

Waziri wa afya wa Mali Fanta Siby ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mama huyo na wanawe wako salama na watakuwa wanarudi nyumbani hivi karibuni.

Picha kwa hisani ya mdhamini.