Maambukizi ya virusi vya corona yamepungua kiasi cha haja na kufikia asilimia 5.2% katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Kenya imeandikisha visa 345 katika ya sampuli 6,686 na kufikisha idadi ya visa hivyo nchini kuwa 160,904.

Idadi ya waliopona imefikia 109,217 baada ya kupona kwa wagonjwa wengine 140.

Wagonjwa 24 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maafa kuwa 2,805.

Jumla ya watu 894,076 wamepewa chanjo ya corona kote nchini ikiwemo watu 275,453 walio na umri wa miaka 58 na zaidi, wahudumu wa afya 158,772, walimu 139,221 na maafisa wa usalama 75,169.