Makachero wa idara ya upelelezi nchini DCI wamenasa noti bandia za dola ya Marekani na pauni ya Uingereza zenye thamani ya shilingi Million 350 mtaani Ruiru kaunti ya Kiambu.

Washukiwa watatu raia wa Cameroon wamekamatwa na makachero hao na inaaminika kuwa ni miongoni mwa genge ambalo limekuwa likiwalgahi wakenya na pesa bandia.

Aidha imebainika kuwa washukiwa, Paulin Francis na Njikam Omar wako humu nchini kinyume cha sheria huku mshukiwa wa tatu Job Kentong akiwa na cheti cha kuwa nchini kama mkimbizi.

Maafisa hao walifanya msako nyumbani kwa mshukiwa mtaani Muthaiga ambapo bastola moja ilipatikana ambayo leseni yake ya umilkiilikuwa imepitwa na wakati.

Bastola hiyo imebainika kuwa ya mshukiwa wa nne Loise Kaguongo ambaye inaaminika amekuwa akitumia biashara yake ya kubadilisha pesa kuwasaidia wakora hao kuwalaghai wakenya.

Washukiwa hao watafikishwa mahakamani pindi baada ya kukamilika kwa uchunguzi.