Shirika la afya duniani (WHO) limeyataka mataifa ya Afrika kuwa macho ili kuepuka wimbi lingine la msambao wa virusi vya corona barani.

Mkurugenzi wa shirika hilo Afrika, Matshidiso Moeti amesema takwimu za hivi punde zinzoenesha kuwa maambukizi hayo yanapungua ila kuna haja ya kuwa makini zaidi.

Ameonya kuwa baadhi ya mataifa yameanza kulegeza kamba katika utekelezwaji wa kanuni za kuzuia msambao wa virusi hivyo jambo analosema ni hatari mno.

Kufikia sasa, mataifa ya Afrika yameandikisha visa milioni 4.5 vya covid-19 ikiwemo maafa 120,000.