Jaji Said Juma Chitembwe amekosoa uamuzi wa mahakama ya upeo wa kutupilia mbali matokeo ya uchaguzi wa Urais wa mwaka 2017.

Katika mahojiano ya kumtafuta jaji wa mahakama ya upeo, jaji Chitembwe ameiambia tume ya huduma za mahakama JSC chini ya uenyekiti wa Olive Mugenda kwamba kwa maoni yake hakuona haja ya kutupilia mbali matokeo hayo.

Jaji huyo pia pia ameiambia JSC kuwa analenga kuhakikisha wakenya wanapata uhuru wao kulingana na katiba bila ya kukandamizwa na sheria zilizopitwa na wakati.

Wa pili kuhojiwa amekuwa jaji D.K Njagi Marete ambaye amependekeza kuongezwa kwa idadi ya majaji wa mahakama ya upeo kutoka saba hadi tisa ili kukabili mrundiko wa kesi mahakamani.

Hapo kesho, itakuwa zamu yao jaji Nduma Nderi wa mahakama ya leba na msomi Dr Patrick Nyaberi Lumumba.

Wengine ambao watahojiwa ni majaji William Ouko, Joseph Sergon na wakili Alice Yano.