Maambukizi ya ugonjwa wa corona yako katika asilimia kumi (10%) huku watu 495 wakikutwa na virusi hivyo katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii ni baada ya kupima sampuli 4,929 katika muda huo na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 158,821.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa watu 242 zaidi wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 108,124 huku maafa 19 zaidi yakidhibitishwa na kufikisha idadi hiyo kuwa 2,707.

Kuhusu shughuli ya utoaji chanjo ya Astrazeneca inayoendelea kote nchini, jumla ya watu 865,897 wamepata chanjo hiyo ikiwemo watu walio na umri wa miaka 58 na zaidi 502,893, wahudumu wa afya 156,344, maafisa wa usalama 72,581, waalimu 134,083.