Chama cha mawakili nchini (LSK) kimekosoa namna mchakato wa kumteua Martha Koome kama Jaji Mkuu ulivyoendeshwa.

LSK kupitia rais wake Nelson Havi kinahoji kwamba tume ya huduma za mahakama JSC iliharakisha kumteua Koome kwa wadhifa huo licha ya kuwepo kwa kesi kadhaa mahakamani kupinga mchakato huo.

Na sasa chama hicho kimetoa makataa ya siku saba kwa JSC kutangaza wazi alama alizopata kila muwaniaji aihojiwa kwa wadhifa huo ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na uwazi kwenye shughuli hiyo.

Na huku mahojiano ya kumtafuta jaji wa mahakama ya upeo yakitazamiwa kuanza wiki ijayo, LSK imetaka shughuli hiyo kuendeshwa kwa uwazi na haki pasipokuwa na maonevu.

Msimamo wa LSK unakuja wakati ambapo bunge linasubiriwa kumsaili Koome baada ya kupokea uteuzi wake kutoka kwa rais Uhuru Kenyatta.