Watu watatu wamefariki na wengine watano kujeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea Makupa, Mombasa Alhamisi asubuhi.

Inaarifiwa kwamba ajali hiyo ilitokea wakati matatu iliruka kizuizi na kugongana na lori.

Matatu hiyo inayobeba abiria 14 ilikuwa safarini kuelekea Changamwe kutoka Makupa wakati ajali hiyo ilitokea majira ya saa moja asubuhi.

Mkuu wa trafiki eneo la Pwani Peter Maina amedhibitisha kutokea kwa  ajali hiyo akisema huenda ilitokea baada ya dereva wa matatu kupoteza udhibiti.