Rais Uhuru Kenyatta amevunja bodi nzima ya shirika la kununua na kusambaza vifaa vya matibabu (KEMSA) kufuatia sakata ya kupotea kwa pesa za kupambana na corona.

Rais Kenyatta amemteua Mary Chao Mwadime kuwa mwenyekiti mpya wa bodi hiyo iliyokuwa inaongozwa na seneta wa zamani wa Murang’a Kembi Gitura.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe wakati uo huo amewateua wanachama wapya wa bodi hiyo akiwemo; Lawrence Wahome, Robert Nyarango, Terry Ramadhani na Linton Kinyua.

Gitura amepewa majukumu mengine mapya ya kuwa mwenyekiti ya tume ya mawasiliano nchini (CA).

Uhamisho wa Kembi Gitura hadi katika tume hiyo umekosolewa na bunge ikizingatiwa kwamba uchunguzi kuhusu sakata ya KEMSA bado unaendelea.