Gavana wa Vihiga Wilber Ottichilo anahojiwa na bunge la Senate kuhusu matumizi ya pesa za kupambana na COVID-19.

Kamati ya bunge hilo kuhusu afya inamhoji Ottichilo kufuatia maswali yaliyoibuliwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za umma.

Haya yanajiri siku moja baada ya kamati hiyo chini ya uenyekiti wake seneta wa Trans Nzoia Michael Mbito kumuuliza maswali gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku kuhusu matumizi ya Shilingi Milioni 265 za kupambana na corona.

Lenku alikuwa na wakati mgumu kuelezea ni vipi aliruhusu kampuni moja kupewa kandarasi ya kusambaza hewa ya oxijeni pasipokuwa na mkataba.