Baraza la magavana limehairisha kongamano la saba la kila mwaka lililokuwa limeratibiwa kuandaliwa kati ya tarehe 23-26 mwezi Agosti mwaka huu katika kaunti ya Makueni kwa sababu ya kuongezeka kwa maambukizi ya corona.

Katika taarifa, mwenyekiti wa baraza hilo gavana Martin Wambora vile vile amelalama kwamba serikali za kaunti zimelewa na zinahitaji pesa zaidi kusaidia katika kupambana na janga la corona.

Miongoni mwa changamoto wanazokabiliana na nazo ni ukosefu wa oxijeni ya kutosha pamoja kupungua kwa vitanda vya wagonjwa mahututi.

Kutokana na hali hiyo, magavana wanateta kuwa wamelazimika kutumia pesa zaidi ambazo hazikuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha vita dhidi ya janga hilo na kutoa wito kwa serikali ya kitaifa kuwapa rasilimali zaidi.