Polisi wa kituo cha Kiogoro eneo bunge la Nyaribari Chache wanamzuilia baba mmoja kwa kudaiwa kuwadhulumu kimapenzi binti zake wawili.

Baba huyo, 32, anasemekana kuwadhulumu wanawe wenye umri wa miaka 12 na 14 tarehe tofauti katika eneo wanakoishi wadi ya Nyankoba, Bobaracho.

Naibu chifu wa eneo hilo Wilfred Nyakeirura anasema uchunguzi wa kimatibabu unaonesha kuwa watoto hao walidhulumiwa kimapenzi na mshukiwa alitekeleza vitendo hivyo wakati mama yao hakuwepo.

Mshukiwa anazuiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani.