Jaji wa Mahakama ya Leba Nduma Nderi amehojiwa na tume ya huduma za mahakama (JSC) kwa nafasi ya jaji Mkuu.

Nderi ametilia shaka jinsi malalamishi dhidi ya majaji yanavyochunguzwa na kusema yanaathiri  utendakazi wa idara ya mahakama.

Jaji Nderi ametetea utendakazi wake katika mahakama ya leba, akisema mabadiliko aliyoleta yamesaidia katika kuharakisha upatikanaji wa haki.

Nderi amiambia JSC kwamba ananalenga kukabili swala la ufisadi katika idara ya mahakama pindi anapochaguliwa kuwa jaji mkuu kwa kuwahusisha washikadau haswa kupitia  vipindi vya redio.

Wengine ambao watahojiwa wiki hii ni wakili Fred Ngatia, jaji William Ouko, Profesa Moni Wekesa na Alice Yano.

Wiki iliyopita, watu watano walihojiwa akiwemo wakili Philip Murgor, Jaji David Marete, jaji Martha Koome, msomi Profesa Kameri Mbote na jaji Juma Chitembwe.

Wadhifa huo ulisalia wazi kufuatia kustaafu kwa David Maraga mapema mwaka huu.